DAMASCUS: Waziri Mkuu wa Irak asema ziara yake nchini Syria ni ya manufaa
22 Agosti 2007Matangazo
Bwana al-Maliki amesema hayo kwa wandishi habari mjini Damascus baada ya mazungumzo yake na rais Bashar al-Assad wa Syria .
Waziri Mkuu huyo wa Irak, yupo nchini Syria kwa ajili ya ziara rasmi ya siku tatu, anayoifanya kwa mara ya kwanza tokea awe waziri mkuu wa Irak.
Bwana al –Maliki amesema nchi yake na Syria zina maslahi ya pamoja na zinapaswa kutatua matatizo kwa pamoja kwa manufaa yao.