1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Danny Jordaan akana madai ya kumbaka mwimbaji Jennifer

John Juma
2 Novemba 2017

Rais wa zamani wa shirikisho la kandanda nchini Afrika kusini, Danny Jordaan, amekana madai kwamba alimbaka mwimbaji  Jennifer Ferguson.

https://p.dw.com/p/2muBO
Präsident der Südafrikanische Fussballverband Danny Jordaan
Picha: picture-alliance/Pressefoto ULMER/M. Ulmer

Rais wa zamani wa shirikisho la kandanda nchini Afrika kusini, Danny Jordaan, amekana madai kwamba alimbaka mwimbaji  Jennifer Ferguson, ambaye alidai mwezi uliopita kwamba alibakwa na kiongozi huyo katika hoteli moja mjini Port Elizabeth baada ya  kufanya tamasha la muziki mwaka 1993.

Ferguson, ambaye ni mbunge wa zamani wa chama tawala cha African National Congress ANC, amesema amehamasishwa na  hashtag "Me Too", ikiwa na maana Hata Mimi, katika kampeni ya mitandao ya kijamii ambayo ilianza baada ya wanawake kadhaa  kudai kwamba walibakwa na mtayarishaji filamu maarufu katika Hollywood Harvey Weistein.

Kubakwa kwa wanawake na watoto ni jambo linalotokea sana nchini Afrika kusini, wakati Umoja wa Mataifa unasema wanawake na  wasichana wanabakwa kila sekunde 26.