1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Demjanjuk awasilishwa Ujerumani

12 Mei 2009

Mtuhumiwa wa kambi ya Manazi kukabili mashtaka.

https://p.dw.com/p/HoRT
John Demjanjuk

Mlinzi wa kambi ya Manazi ya kuwahilikisha wayahudi John Demjanjuk, amewasilishwa leo Ujerumani kutoka Marekani ili kukabili mashtaka kwa tuhuma za kusaidia kuhilikishwa mayahudi 29,000 wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia hapo 1943.

Mashtaka ya Demjanjuk, yaweza kufungua mlango wa hukumu ya mwisho kubwa kabisa ya Manazi tangu kumalizika vita vikuu vya pili vya dunia.Kwa muujibu wa shirika la habari la Reuters, ndege ya mtuhumiwa John Demjanjuk,ilitua katika Uwanja wa ndege wa Munich leo asubuhi na mara kutua, magari ya polisi na ya kupakia mgonjwa yaliizunguka ndege hiyo.Mshtaki mkuu wa jiji la Munich baadae alithibitisha kuwasili mtuhumiwa.

"Amewasili" alisema Bw. anton Winkler wa afisi ya mshtaki.

Demjanjuk,mstaafu alietumikia kiwanda cha magari nchini Marekani,alipigana sana kuzuwia kuletwa Ujerumani lakini mwishoe,mahkama za Marekani zilikataa rufaa alizokata.Hatahivyo, mzee huyo mwenye umri wa miaka 89 na ambae yuko usoni kabisa mwa orodha ya watu 10 wanaosakwa na Taasisi ya Simon Wesenthal kwa tuhuma za uhalifu,huenda juu ya hivyo akaonekana si mzima wa afya kumudu kakabili vishindo vya mashtaka mahkamani.

Demjanjuk, mzaliwa wa Ukraine ,amekanusha kuhusijka kwa aina yoyote ile katika msiba wa holocaust-msiba wa kuwahilikisaha mayahudi.Akidai aliandikishwa katika jeshi la uruasi hapo 1941 na halafu akawa mateka na mfungwa wa vita wsa wajerumani na halafu akatumika katika kambhi ya wafungwa ya wajerumani hadi 1944.

Hakimu wa Ujerumani mjini Munich, alitoa waranti wa kukamatwa Den mjanjuk hapo mwetzi Machi, mwaka huu ili kushtakiwa kwa kusaidia kuhilikishwa hadi mayahudi 29,000 katika kambi ya kuhilikisha ya Sobibor enzi za vita vya pili vya dunia.

Kutoka uwanja wa Ndege wa Munich, John Demnjanjuk akitazamiwa kupelekwa moja kwa moja katika gereza liliopo karibu na Munich.Wakili wake mjini humo,Guenther Maull, alisema atamshauri mtuhimiwa kutosema lolote.

Demjanjuk alipokonywa uraia wa Marekani baada ya kutuhimiwa hapo 1970 kuwa yeye ndie yule "Ivan the Trerrible"-mlinzi-mtesaji mkubwa wa kambi ya vifo ya Treblinka.

Demjanjuk alisafirishwa kwa nguvu kupelekwa Israel 1986 na akapitishiwa adhabu ya kifo 1988.Hii ilikua baada ya wale walionusurika na msiba wa "holocaust " kumtambulisha kuwa ndie mlinzi dhaifu mkubwa wa kambi ya Treblinka.Lakini, Mahkama Kuu ya Israel , ilifuta hukumu aliopewa huko pale ushahidi mpya ulipobainisha yamkini ni mtu mwengine mwenye jina hilo la "Ivan." na sio yeye.

Halfu akapewa tena uraia wake wa Marekani hapo 1998 lakini, wizara ya sheria ya Marekani ikaifungua upya kesi yake hapo 1999 ikidai aliwatumikia manazi kama mlinzi wa kambi yao katika kambi 3 nyenginezo na ameficha hayo.Uraia wake wa Marekani ukafutwa tena 2002.

Muandishi: Ramadhan Ali/ RTRE

Mhariri: Mohammed AbdulRahman