1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DILI: Uchaguzi wa rais Timor ya Mashariki

9 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3t

Uchaguzi wa rais unafanywa hii leo nchini Timor ya Mashariki.Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel,Jose Ramos-Horta na mgombea wa chama tawala,Francisco Guterres wanapambana katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais.Mwezi uliopita katika duru ya mwanzo,hakuna aliepata uwingi wa kuweza kushinda moja kwa moja.Kiasi ya raia 500,000 wana haki ya kupiga kura kumchagua rais mpya.