1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DOUALA:Ndege ya abiria ya Kenya Airways imeanguka nchini Cameroun

5 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC4a

Radio ya taifa ya Cameroun imeripoti kwamba ndege ya abiria ya shirika la Kenya Airways iliyokuwa na watu 114 imeanguka karibu na mji wa Niete kaskazini mwa Kamerun.

Ndege hiyo iliyotokea Abidjan, ilikuwa inaendelea na safari yake kutoka Douala Cameroun kabla ya mawasiliano kukatika.

Ilikuwa inaelekea Nairobi ambapo ilitarajiwa kuwasili saa 12 na nusu leo asubuhi.

Mkurugenzi wa shirika la Kenya Airways bwana Titus Naikuni amesema kuwa timu za waokoaji zimefika mahala ilipoangukia ndege hiyo karibu na mji wa Niete kaskazini mwa Cameroun.