1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Draghi, Macron na Scholz kuzuru Kiev?

Bruce Amani
15 Juni 2022

Je, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz atakwenda Ukraine na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi? Matarajio ni makubwa na ziara hiyo ya Kiev imekuwa ikisuburiwa kwa muda mrefu.

https://p.dw.com/p/4CkcC
Kombo | Links Mario Draghi | Mitte Emmanuel Macron | Rechts Olaf Scholz
Picha: Francois Mori/Michael Kappeler/AP Photo/dpa/picture alliance

Huku vita vya Urusi nchini Ukraine vikiendelea kupamba moto, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amekuwa kila mara akitoa wito kwa nchi za Magharibi kusimama nae na kuonyesha mshikamano dhidi ya Rais Vladmir Putin wa Urusi. Je, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz atakwenda Ukraine na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi? Matarajio ni makubwa na ziara hiyo ya Kiev imekuwa ikisuburiwa kwa muda mrefu. Ripoti imeandikwa na Sabine Kinkartz na Christoph Hasselbach wa DW

Balozi wa Ukraine nchini Ujerumani Andrij Melnyk, anafahamika sana kwa kutumia maneno makali ya uokosoaji. Wakati Habari zilivuja kuwa Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz atakwenda Kiev Pamoja na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi, Melnyk aliweka picha kwenye Twitter, ya vifaru vitano vya kivita na kuandika ujumbe ulioelekezwa kwa serikali ya Ujerumani. Hapa naunukuu: "Kwa nini mnalinyima jeshi la Ukraine magari haya ya kivita, yanayoweza kuwasilishwa mara moja na kampuni ya Rheinmetall, wakati Ukraine inawmaga damu katika eneo la Donbass mkiona na macho yenu?”

Ukraine | Wolodymyr Selenskyj und Annalena Baerbock in Kiew
Picha: Ukrainian Presidential Press Off/AP/dpa/picture alliance

Muda mfupi baadae, Melny akazungumza na vyombo vya Ujerumani. ''Maoni yetu ni kuwa hasa kwa wakati huu, ambapo Warusi wanafanya mashambulizi haya makubwa ya umwafaji damu katika eneo la Donbas kwa wiki nyingi tumewapoteza wanajeshi wengi sana na tunahitaji sasa hivi silaha hizi nzito kutoka Ujerumani. Na ni vifaru hasa vya Leopard 1 lakini pia Leopard 2 na magari makubwa ya kivita. Ujerumani iko tayari kuleta zana hivi mara moja bila kutumia ujanja wowote au kupitia njia za mkato.''

Katika mahojiano na televisheni ya ZDF, Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema wanamhitaji Scholz ili kuwa na uhakika kuwa Ujerumani inaiunga mkono Ukraine. Yeye na serikali yake wanafaa kufanya uamuzi.

Soma pia:Zelensky: Mataifa ya Magharibi hayaungana kuisaidia Ukraine

Matarajio yako juu kwa ziara hiyo ya Ukraine ya viongozi watatu wa serikali, ambayo haijathibitishwa na Ujerumani. Labda kwa sababu pia kansela amechukua muda mrefu kufanya uamuzi. Scholz alipata mualika wa kwenda Kiev kitambo. Mara ya kwan za hatahivyo hakuukubali. Sababu ilikuwa serikali ya Ukraine ilikuwa imefuta mwaliko wa Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier mwezi Aprili kwa sababu ilisemekana alikuwa karibu sana na Kremlin.

Deutschland | Bundeswehr übt Truppenverladung | Bergepanzer vom Typ Leopard 1
Picha: Soeren Stache/dpa/Zentralbild/picture alliance

Steinmeier alitaka kuitembelea Kiev, lakini hakuruhusiwa. Scholz aliruhusiwa, lakini hakutaka. Scholz kisha alifanya mazungumzo na Zelensky na kuyaweka mambo sawa. Lakini hata baada ya hilo, Scholz akasema kuwa hawezi kujiunga na kundi la watu kwa ziara fupi ya kuingia na kutoka na kupigwa tu picha.

Henning Hoff wa Baraza la Mahusiano ya Kigeni la Ujerumani ameiambia DW kuwa sasa ni wakati wa maneno kuwekwa katika vitendo.

Scholz kwa mara nyingine amekataa tuhuma kuwa anasita kutoa msaada kwa Ukraine. ''Kila kitu kimeshatangazwa. Tutapeleka silaha zote ambazo tumetangaza. Zipo tayari viwandani na zinatayarishwa ipasavyo. na jeshi ndilo linahusika. Mazoezi yanaendelea kwa sasa na nadhani lingekuwa jambo zuri kama mtu mmoja au mwingine angefikiria kwanza mara mbili kabla ya kutoa maoni yake kuhusu suala moja au jingine.''

Kwenye mkutano mjini Vilnius wiki iliyopita na wakuu wa mataifa na serikali za Lithuania, Latvia na Estonia, Scholz alihisi jinsi hotuba zisizo na vitendo zinavyochukuliwa Mashariki mwa UIaya. Jamhuri hizo za zamani za uliokuwa Muungano wa Kisovieti zinahofia kuwa huenda zikawa waathiriwa wajao wa uchokozi wa Urusi kama Putin atafulu nchini Ukraine.

Scholz mara kwa mara anatumia fomyula ya "Lazima Urusi isishinde vita hivi.” Anajiepusha kusema Ukraine lazima ishinde vita hivi.

Viongozi wengi wa Ulaya Mashariki wanakosoa sana mazungumzo ya Pamoja ya simu kati ya Scholz na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Urusi Valdmir Putin – bila kuwahusisha washirika wengine. Macron alionya mara kadhaa kuwa Urusi haipaswi kudhalilishwa na kuwa Putin anapaswa kuambiwa uso kwa uso aachane na vita. Rais wa Lithuania Gitanas Nauseda alisema mbele ya Scholz kuwa ni vigumu sana kufanya mazungumzo na dikteta.

Bundespräsident Steinmeier in Rottweil
Picha: Silas Stein/dpa/picture alliance

Ukraine na nchi nyingine za Mashariki mwa Ulaya zinakosa kitu kingine kutoka kwa Scholz: ahadi ya wazi kwa mtizamo Ukraine kuhusu wa Umoja wa Ulaya. Gazeti la Neue Zürcher liliandika mwezi Juni kuwa umuhimu wa ahadi ya aina hiyo unakwenda mbali na matarajio ya kuwa mwanachama wa umoja huo.

Vyombo vya habari vya Kiingereza na Kifaransa kwa upande mwingine, katika siku za karibuni vimekuwa rafiki tena kwa Scholz. Gazeti la Economist la Uingereza liliandika "Kinyume na matukio ya historia yake na historia yake ya kisiasa, Ujerumani inaisaidia Ukraine zaidi ya ilivyotarajiwa na wengi.

Henning Hoff wa Baraza la Ujerumani kuhusu Mahusiano ya Kigeni anatoa tathmini ya mchanganyiko. "Katika sera ya usalama na ulinzi ya Ujerumani, labda mengi yametokea katika miezi mitatu iliyopita kuliko kaika miongo mitatu, yakiungwa mkono na raia wake wengi.”

Kutoka kwa mtizamo wa washirika, hata hivyo, Ujerumani ndio sasa tu imewasili katika nyakati za sasa. Lakini mengi yanatarajiwa kwa nchi hiyo: Kutwaa jukumu la uongozi kwa uwazi zaidi kuliko ilivyokuwa.”

Pamoja na Ufaransa na Italia? Kama kweli itafanyika, ziara ya Kiev ya Olaf Scholz, Emmanuel Macron na Mario Draghi itahusishwa na matarajio makubwa. Kama yatatimizwa itasubiriwa kuona.

Makala hii awali iliandikwa katika Kijerumani