1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC kabla ya uchaguzi yatakiwa kuwa na utulivu

Sekione Kitojo
19 Desemba 2018

Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa limezitaka pande zote zinazohusika katika uchaguzi katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kupinga matumizi ya nguvu na ghasia siku tano kabla ya uchaguzi wa rais nchini humo.

https://p.dw.com/p/3AMet
DRCONGO-POLITICS-KABILA
Picha: Getty Images/AFP/J. D. Kannah

Jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya  Congo itafanya uchaguzi  wake uliocheleweshwa kwa  muda  mrefu ambao  utashuhudia  ubadilishanaji  wa  madaraka  kwa njia  ya  amani  kwa  mara  ya  kwanza  tangu  nchi  hiyo kupata  uhuru  kutoka  Ubelgiji. 

Demokratische Republik Kongo | Emmanuel Ramazani Shadary, Präsidentschaftskandidat in Kinshasa
Mgombea wa chama tawala katika DRC Emmanuel Ramazani ShadaryPicha: Getty Images/AFP/J. Wessels

Kiasi  watu  sita  wameuwawa  katika  ghasia  zilizojitokeza katika  utawala  wa  miaka  17  wa  Rais  Joseph Kabila. Serikali  ya  nchi  hiyo  inakana  kuhusishwa  kwa  njia yoyote  na  mauaji  hayo  pamoja  na  kampeni. Baraza  la Usalama  limezitaka  pande  zote  kuendelea  kupinga ghasia  za  aina  yoyote, na  kujizuwia  kwa  kiwango  cha juu  kabisa  katika  hatua  wanazozichukua na  kujitenga na  kuchochea  ghasia  na  hotuba  za  uchochezi  na kutakiwa  kutoa  maelezo  ya  tofauti  zao  kwa  njia  za amani, imesema  taarifa  ya  baraza  hilo.

Wajumbe  wa  baraza  la  Usalama  pia  wamesisitiza umuhimu  wa  kuhakikisha  usalama  na  ulinzi  kwa wagombea  na  wapiga  kura  wakati  wa  kipindi  cha kampeni.
 

Wakati  huo  huo, wamerejea  wito  wao  kwa  vyama  vyote kufanyakazi  kwa  amani  na  kwa  njia  nzuri  katika mchakato  wa  uchaguzi, kuhakikisha  uwazi, matokeo  ya amani na  yenye  kuaminika.

Demokratische Republik Kongo Polizei
Polisi wa DRC wakilinda doriaPicha: Getty Images/AFP/M. Mulopwe

Hatua zimepigwa katika kuelekea  uchaguzi

"Wakati  wanakaribisha  hatua  zilizopigwa  katika matayarisho  ya  kiufundi  kwa  ajili  ya  uchaguzi  huo, wajumbe  wa  baraza  la  Usalama  la  Umoja  wa  mataifa wana  wasi  wasi  juu  ya  kile  walichokieleza  kuwa  ni matukio  ya  ghasia  yanayochafua  siku  za  mwisho  za kampeni  za  uchaguzi, taarifa  yao  ilisema. Kwa  hiyo baraza  hilo  linatoa  wito kwa  serikali  ya  DRC  kufanya uchunguzi  wa  haraka  kuhusiana  na  matukio  hayo, taarifa  hiyo  imesema.
 

Katika  kuelekea  katika  uchaguzi  huo  siku  ya  Jumapili tarehe  23, kuanzia  mataifa  yenye mpaka  pamoja  na Jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya  Congo, baadhi  yake  yakiwa yamechochea  mizozo  ya  nchi  hiyo,  mataifa  makubwa ya  kimataifa  kujaribu  kufanya  juhudi  za  kuleta  amani , athari  za  uchaguzi  ujao, mitikisiko  katika  nchi  hiyo inaonekana kufika  mbali  zaidi.

Mataifa jirani  ya  taifa  hilo  yamepigana  vita  katika  ardhi ya  Jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya  Congo, lakini bado  taifa hilo  linalinda  maslahi  yake katika  taifa  hilo  lenye matatizo.
 

Utawala  wa  sasa  katika  DRC  ni  matokeo  ya  moja  kwa moja  ya  uingiliaji  kati  wa  mataifa  jirani  katika  mizozo miwili  kati  ya  mwaka  1996  na 2003  ambayo imesababisha  kuingizwa  nchini  humo  majeshi  kutoka karibu  mataifa  saba  ya  Afrika  na  kusababisha mamilioni  ya  watu  kuuwawa.
 

Demokratische Republik Kongo Wahlkampagne Felix Antoine Tshilombo Tshisekedi in Bukavu
Mkutano wa kampeni wa mgombea Felix Antione Tshilombo Tshisekedi mjini BukavuPicha: Lydie Omanga

Moto wa  eneo  hilo uliwashwa  na  mauaji  ya  kimbari nchini  Rwanda  mwaka  1994, wakati  kiasi  ya  wakimbizi wengi  wao  wakiwa  ni  wahutu karibu  milioni  mbili pamoja  na  wale  ambao  waliongoza  mauaji  hayo , walipokimbilia  ndani  ya  Congo. Waasi walitumia  kambi zao  kama  vituo  vipya  vya  kufanya  mashambulio  yao dhidi  ya  Rwanda , na  kusababisha  Rwanda  kuivamia Congo.
 

Rwanda  kwa  msaada  wa  Uganda , iliunga  mkono  uasi ambao  ulisababisha  kuangushwa  kwa   Rais  Mobutu Sese  Seko  na  kushuhudia  Laurent Desire kabila  kuwa rais  mwaka  1997. Haikuchukua  hata  mwaka  mzozo mwingine  ukaibuka.

Mwandishi: Sekione Kitojo/afpe

Mhariri: Mohammed Khelef