1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DRC yathibitisha visa viwili vya ugonjwa wa Ebola

Tatu Karema
11 Februari 2021

Wizara ya Afya katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imesema Alhamisi kuwa watu wawili wameambukizwa ugonjwa wa Ebola na kufariki dunia ndani ya wiki hii katika jimbo la Kivu Kaskazini.

https://p.dw.com/p/3pDPs
Kongo: Erneuter Ausbruch von Ebola
Picha: Reuters/G. Tomasevic

Taarifa ya wizara hiyo imesema mwanamke mmoja aliyefariki jana Jumatano katika wilaya ya Biena alikuwa na ukaribu na mwanamke mwingine ambaye pia alikufa baada ya kuambukizwa Ebola. Wizara ya afya ya DRC tayari imepeleka jopo la waatalamu wa afya kwenda eneo hilo na inawafuatilia zaidi ya watu 100 waliokutana na wanawake hao wawili katika wilaya za Biena na Katwa.

Mlipuko mkubwa wa ugonjwa wa Ebola uliikumba DRC kati ya mwaka 2018 na 2020 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 2,200 ya kutangazwa kuwa umedhibitiwa mwezi Juni mwaka uliopita.