1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DUBAI: Tawi la al-Qaeda lajitambulisha na shambulizi jipya

22 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNj

Tawi la Al-Qaeda katika Afrika ya Kaskazini limesema kuwa limehusika na shambulizi la kujitolea muhanga la siku ya Ijumaa,nchini Algeria.Msafara wa magari ulishambuliwa mashariki ya mji mkuu Algiers.Mripuko huo ulijeruhi Waalgeria 6,Wafaransa 2 na Mtaliana mmoja.

Mwanzoni mwa mwezi huu pia,tawi la Al-Qaeda la Afrika ya Kaskazini,lilijitambulisha kuhusika na mashambulizi mengine mawili nchini Algeria. Mashambulizi hayo yaliua zaidi ya watu 50.