1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Duru ya 3 ya Champions League

20 Oktoba 2008

Bayern munich mabingwa wa ujerumani wana miadi kesho na Fiorentina-Manchester na celtic.

https://p.dw.com/p/FdgZ

Baada ya mapumziko ya wiki 2,kinyanganyiro cha champions-League-kombe la klabu bingwa barani Ulaya,kinarudi uwanjani leo.

Mabingwa wa kombe hilo Manchester united, wanacheza leo nyumbani na mahasimu wao wakiwa waskochi Celtic Glasgow katika changamoto za kundi E.Chelsea ina miadi na AS Roma.Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wakiongoza kundi F, wana miadi na Fiorentina ya Itali wakati wenzao Werder Bremen wakiwa kundi B wanawatembelea Panathaniakos huko Ugiriki.

Ramadhan ali anawafunulia zaidi kawa la changamoto za kati ya wiki hii za kombe hilo la klabu bingwa barani Ulaya:

Mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich wanaingia uwanjani wakitiwa moyo na ushindi wa dakika za mwisho jumamosi katika Bundesliga dhidi ya Karlsruhe.Mahasimu wao katika duru hii ya 3 ya Champions League ni Fiorentina ya Itali ambayo bila shaka imesikia misukosuko ya kocha Klinsmann tangu ashike usukani wa mabingwa hawa wa Ujerumani. Isitoshe, Munich imeshindwa kutamba nyumbani katika mapambano 4 yaliopita ya kinyanganyiro cha kombe la ulaya na imetoka sare mechi 3 zilizopita kwa bao 1:1.Dhidi ya klabu za Itali, Bayern Munich imeshinda mechi 1 kati ya 6 nyumbani ilipocheza dhidi ya klabu za itali.

Kwa upande wake Fiorentina, haikutamba hata mara moja ilipotembelea Ujerumani mara 3 zilizopita tena mnamo miaka 20 iliopita.Fiorentina ilitoka sare na Werder Bremen katika nusu-finali ya 1989 ya kombe la ulaya la UEFA.

Werder Bremen zamu yao ni kesho ikiatumai kutamba mbele ya wagiriki Panathaniakos .Bremen ilimudu suluhu ya mabao 3:3 na Borussia Dortmund mwishoni mwa wiki.

Mabingwa Manchester United ya uingereza wanapimana nguvu leo na wenzao kutoka scotland-Celtic.Hakuna sababu kwa Celtic kuweka matumaini ya kuweza kutamba leo mbele ya Manchester huko old Trafford,kwani jogoo la Manchester Wayne Rooney,linazidi kuwa hatari na yamkini likawika tena hii leo.

Celtic imepoteza mechi 17 kati ya 18 iliocheza ngambo na pia wachezaji wake maarufu wameumia.Baada ya kuanza pole pole kwa kutoka suluhu 0:0 na Villareal ya Spain ,Manchester sasa iko tayari kutamba tena.kwani imetiwa shime na ushindi wake uliopita ilipopambana na Aalborg ya Denmark wa mabao 3-0. Celtic ina pointi 1 tu kutoka mechi zao 2 zilizopita.Na ni kama kupanda mlima ikiwa Celtic yataka kusonga mbele katika duru ijayo ya timu 16.

Mpamba no mwengine wa kukata na shoka ni kati ya mabingwa wa Spian Real Madrid na Juventus turin ya Itali.Real imeshindwa mara 2 katika mechi zake 28 zilizopita nyumbani lakini mechi yao ya mwisho mjini Madrid dhidi ya timu ya Itali ilimalizika kwa kushindwa Real mabao 2-1 na AS Roma.Mara hii yamkini timu hizi mbili zikatoka suluhu. Juventus imeshinda mechi 2 tu kati ya 10 ngambo .

Arsenal ina miadi na Fenerbahce ya Uturuki.Arsenal haikutiwa bao katika mechi 3 zilizopita dhidi ya klabu ya Uturuki na inakusudia kubakia hivyo mara hii.Na katika mapambano jumla ya ulaya, Arsenal imeshinda mapambano 12 kati ya 18 ngambo kwenye vikombe vya Ulaya.

Fernerbahce ,ambayo haikushindwa jumla ya mechi e 15 zilizopita nyumbani na imeshinda 11 kati ya hizo, imetamba katika mechi zake 2 zilizopita za kombe hili la Ulaya dhidi ya timu za Uingereza.Iliikomea Chelsea 2-1 katika robo-finali ya msimu uliopita na halafu Manchester United kwa mabao 3-0 miaka 4 nyuma.lakini,mla ni mla leo,mla jana kala nini.

Mashabiki wanangojea kwa hamu firimbi basi kulia kwa duru nyengine ya champions League.