1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DW yaandaa Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari

Oumilkheir Hamidou
24 Mei 2019

Kuanzia Mei 27- 28 DW inaandaa kwa mara nyengine tena Kongamano la Kimataifa la Vyombo vya Habari au GMF mjini Bonn, Ujerumani. Kauli mbiu ya kongamano la 2019 ni "Shifting Powers"  au "Badilisha Madaraka".

https://p.dw.com/p/3J2ne
Banner zur Bewerbung des Global Media Forum mit Thema, Datum und Ort

Shifting Powers au "Badilisha Madaraka, kauli mbiu hiyo imechaguliwa kwa kuzingatia umuhimu wa mfumo wa digitali katika uwiano kati ya vyombio vya habari, siasa na jamii katika maeneo chungu nzima ya dunia."Wanaojipendekeza  wa kutoka tabaka zote wanatishia uwepo wa Umoja wa ulaya" amesema mkurugenzi mkuu wa DW Peter Limburg."Udhibiti wa habari kimegeuka kuwa  chombo chao cha kudhibiti madaraka."Wakati huo huo wanasiasa wengi wanaeneza risala zao wenyewe naiwe kwa kudhibiti vyombo vya habari vya serikali au kwa kutaangaza habari za uowongo mitandaoni."Uhuru wa mtu kutoa maoni yake umeingia hatarini".

Kongamano hilo la siku mbili linalofanyika kwa lugha ya kiengereza litajitahidi kuwafumbua macho  washirika kuhusu mabadiliko hayo makubwa."Kwa pamoja na pamoja na mashirika kadhaa ya habari ya kimataifa, kwa msaada wa waashirika na wanaotuunga mkono, tutashadidia na kuwagutua waatu wengi zaidi" amesema mkurugenzi mkuu wa DW, Peter Limburg.

Kwa namna hiyo rais wa shirikisho Frank-Walter Steinmeier amepengiwa kujiunga mubashar na mkurugenzi mkuu wa DW kufungua kongamano hilo. Baadae katika juopo la kwaanza la mazungumzo mada itajikita na suala kwa jinsi gani taswira ya vyombo vya habari imebadilika na wapi zinakutikana faida na hatari za mabadailiko hayo. Miongoni mwa watakaohutubia jopo hilo ni pamoja na muasisi mwenza wa kundi la India Today, Aroon Ourie, na Mark Peters wa kampuni la Google. Mkuu wa shirika la uchapishaji la Axel-Springer la Ujerumani, Mathias Döpfner na mwasisi wa mfumo wa digitali, mmarekani Jaron Lanier.

78 | Session | Digitalization and polarization of the media: How to overcome
Kikao cha Kongamano la Vyombo vya Habari 2018, Bonn, UjerumaniPicha: DW/F. Görner

Vyombo vya habari na vyama vya kisiasa

Mnamo siku ya pili ya kongamano la kimataifa la vyombo vya habari-Global Media Forum-GMF mada zote hizo zitajadiliwa upya na kumulika zaidi uhusiano kati ya vyombo vya habari na vyama vya kisiasa. Can Dünder, mhariri mkuu wa zamani wa gazeti la Uturuki, Cumhuriyet atakutana katika meza ya majadiliano pamoja na mkuu wa shirika la utafiti la vituo vya matangazo vya NDR, WDR na gazeti la Sddeutsche Zeitung, Georg Mascolo na wengineo kuzungumzia kondo wa uhusiano huo .

Mada nyengine kadhaa zitajadiliwa katika mikutano ya vyombo vya habari wakishiriki watu 2000 kutoka nchi 140 ikiwa ni pamoja na mustakbali wa uandishi habari wa kikanda. Jumla ya haafla 79 zitafanyika mnamo muda wa siku mbili za kongamano la kimataifa la vyombo vya habari-GMF. Mojawapo ya majopo hayo itajadiliwa mifano bora inayobainisha licha ya mizozo iliyokithiri, ripoti za waandishi habari hazidhuriki.

Kama ilivyo kawaida kila mwaka, kilele cha kongamano la kimataifa la vyombo vya habari ni tuzo ya DW ya uhuru wa mtu kutoa maoni yake..Tuzo ya mwaka huu atatunukiwa mwandishi habari wa Mexico Anabel Hernandez, anaendesha mapambano dhidi ya rushwa, udanganyifu na hali ya kutoadhibiwa wahalifu na ambae amelazimika kuihama nchi yake.