1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

EU yafikiria kuliwekea vikwazo jeshi la Walinzi wa Iran

Lilian Mtono
22 Aprili 2024

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Hadja Lahbib amesema hii leo kwamba vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya kwa Iran baada ya kuishambulia Israel vinatakiwa kukihusisha Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran.

https://p.dw.com/p/4f2aQ
Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran
Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi wa IranPicha: Iranian Supreme Leader's Office via ZUMA Press Wire/picture-alliance

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji Hadja Lahbib amesema hii leo kwamba vikwazo vipya vya Umoja wa Ulaya kwa Iran baada ya kuishambulia Israelvinatakiwa kukihusisha Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi wa Iran.

Lahbib amewaambia waandishi wa habari kabla ya mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje na ulinzi wa Ulaya huko Luxembourg kwamba bado hakuna makubaliano juu ya msingi hasa wa kisheria utakaotumika ili kuwaingiza wahusika hao kwenye orodha ndefu ya umoja huo ya taasisi inazozitaja kuwa za kigaidi.Rais wa Iran alisifu jeshi kulipiza kisasi kwa Israel

"Waziri wa Mambo ya Nje wa Ubelgiji: ''Tutaangazia vikwazo vipya ambavyo kwanza vitahusisha Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi, dhidi ya Iran kama msambazaji na mzalishaji wa droni ambazo pia tumeziona kwenye makumbusho ya kivita ya Ukraine. Lakini pia nadhani tunatakiwa kuviongeza vikwazo dhidi ya wavamizi kwenye Ukingo wa Magharibi. Tutajitahidi kuweka usawa ili tusilaumiwe kwa kwa undumilakuwili.''  

Mawaziri hao wako Luxembourg kujadiliana juu ya msaada kwa Ukraine baada ya bunge la Marekani kuidhinisha karibu dola bilioni 61, pamoja na vikwazo dhidi ya Iran kufuatia shambulizi dhidi ya Israel na hatua yake ya kuisaidia Urusi kijeshi.