1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FIFA kumchunguza rais wa shirikisho la soka la Uhispania

Lilian Mtono
24 Agosti 2023

Shirikisho la Soka Ulimwenguni, FIFA, limefungua kesi hii leo dhidi ya rais wa shirikisho la Soka la Uhispania aliyeibusu midomo ya mchezaji mmoja wakati wakishangilia ubingwa wa michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake.

https://p.dw.com/p/4VXoy
FIFA Fußball Frauen-WM | Luis Rubiales küsst Jennifer Hermoso
Picha: Noe Llamas/Sport Press Photo/ZUMA Press/picture alliance

Kamati ya Maadili ya FIFA imesema itaangazia ikiwa Luis Rubiales alikiuka kanuni za msingi za mwenendo mzuri na kama kitendo hicho kimeuchafua sio tu mchezo wa soka, bali pia shirikisho hilo.

Rubiales alimbusu mchezaji Jenni Hermoso midomoni wakati wa hafla ya kukabidhiwa kombe na medali, baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya England katika fainali za michuano hiyo iliyomalizika Jumapili iliyopita huko Sydney, Australia.