1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Finland yatumai kukubaliana na Uturuki kuhusu NATO

Amina Mjahid
17 Mei 2022

Rais wa Finland Sauli Niinisto leo amesema ana matumaini Finnland na Sweden zitafanikiwa kuungwa mkono na Uturuki katika maombi yao ya kutaka kujiunga na jumuiya ya kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/4BQL5
Helsinki | Pressekonferenz zum Beitritt Nato Mitgliedschaft Finnland | Sauli Niinistö
Picha: Heikki Saukkomaa/Lehtikuva/dpa/picture alliance

Rais wa Uturuki Recep Tayip Erdogan ametishia kuzuia utanuzi wa jumuiya hiyo akizituhumu Finnland na Sweden kwa kuwaficha wanamgambo wa kituruki wa chama cha Kurdistan Workers, ambao wameendeleza uasi wa miongo kadhaa dhidi ya dola la Uturuki. 

Sweden imesitisha uuzaji wa silaha kwa Uturuki tangu 2019 kuhusiana na harakati ya kijeshi ya Uturuki katika nchi jirani ya Syria.

Wakati hayo yakiarifiwa, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock amesema ana imani Finnland na Sweden zitajiunga haraka na NATO licha ya upinzani kutoka kwa Uturuki.

Baerbock aidha amesema ikiwa mchakato utachelewa wanachama wa NATO watazipa nchi hizo hakikisho maalumu la usalama.

Chanzo: reuters