1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Florian Wirtz haondoki Leverkusen msimu ujao

Josephat Charo
31 Machi 2024

Mchezaji kiungo wa klabu ya Bayerl Leverkusen na timu ya taifa ya soka ya Ujerumani, Florian Wirtz hataondoka Leverkusen msimu ujao. Wirtz ametoa mchango muhimu kwa timu yake katika msimu huu wa Bundesliga.

https://p.dw.com/p/4eIVz
Florian Wirtz, kiungo wa Bayern Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani.
Florian Wirtz, kiungo wa Bayern Leverkusen na timu ya taifa ya Ujerumani.Picha: Fabian Bimmer/REUTERS

Mchezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani Florian Wirtz ataendelea kuichezea Bayer Leverkusen msimu ujao kwa "uhakika wa asilimia 100," kwa mujibu wa Afisa Mkuu Mtendaji, Fernando Carro.

"Ukweli kwamba kocha Xabi Alonso anabaki ni kichochea cha ziada kufanya Wirtz asiondoke," Carro aliiambia radio ya Uhispania, Onda Cero, katika mahojiano yaliyotangazwa leo Jumapili.

Wirtz ana mkataba na Leverkusen hadi Juni 2027, lakini vilabu kadhaa vikubwa vimeonesha nia ya kutaka kumsajili.

"Usimamizi wa klabu ya Leverkusen inataka kuibakisha sehemu kubwa ya kikosi cha sasa na kuepuka kulazimika kulipa fidia kwa wachezaji wengi kuondoka kama ilivyokuwa mwaka 2001 na 2002," alisema Carro, ambaye hata hivyo anatarajia ofa nzuri nzuri zenye donge nono.

Lengo lake ni kwa timu kujiimarisha miongoni mwa timu 16 bora barani Ulaya na icheze ligi ya mabingwa Ulaya, Champions.

Leverkusen iko kileleni mwa ligi ya Bundesliga ikiwa mbele ya Bayern Munich kwa alama 13, huku mechi saba zikiwa zimesalia msimu kukamilika. Wanahitaji ushindi wa mechi tatu tu kutwaa ubingwa wa ligi bila kujali matokeo watakayoyapata Bayern.

Timu imekuwa na "msimu mzuri sana" kwa sehemu shukurani zimwendee kocha Alonso. "Hatungeweza kupata matokeo mazuri zaidi," alisema Carro.

Alonso alisema siku ya Ijumaa kwamba atabaki kuwa kocha wa Leverkusen msimu ujao, licha ya vilabu vyake vya zamani Bayern Munich, Liverpool na Real Madrid kuonesha nia ya kutaka kumsajali.

(dpa)