FLORIDA: mwanafunzi ashambuliwa na papa dume!
19 Agosti 2007Matangazo
Mwanafunzi mmoja wa chuo alieshambuliwa na papa ameshonwa mara 100 ili kutibu majeraha 17. Wataalamu wanatuhumu kuwa mwanafunzi huyo ,mwanamke alieponea chupuchupu alishambuliwa na papa dume.
Meno ya papa huyo yalikaribia mapafu ya mwanafunzi huyo lakini alibahatika kwamba mnyama huyo hakuweza kuvishambulia viungo muhimu vya mwili wake.