1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREE TOWN:Wafuasi wa chama cha tawala cha zamani washambuliwa

20 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBO9

Kumekuwa na taarifa za mashambulizi kadhaa dhidi ya wafuasi wa chama tawala cha zamani nchini Sierra Leone cha SLPP.

Wafuasi hao walianza kushambuliwa hapo siku ya Jumatatu baada ya kiongozi wa upinzani Ernest Bai Koroma alipoapishwa kuwa Rais mpya wa nchi hiyo kufuatia ushindi wake kwenye uchaguzi mkuu.

Rais Koroma ameelezea fujo hizo zinazofanywa na wafuasi wake kuwa ni tukio la bahati ambaya, ambapo amelitaka jeshi la polisi kutumia uwezo wake wote kuwakamata wahusika.

Rais huyo alikutana na mawaziri wa serikali iliyopita ambapo aliwahidi usalama.