1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

FREETOWN : Leo ni marudio ya uchaguzi wa rais

8 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBRz

Wananchi wa Sierra Leone leo wanapiga kura katika marudio ya uchaguzi wa urais yanayompambanisha mgombea wa upinzani aliekuwa akiongoza duru ya kwanza Ernest Bai Koroma dhidi ya Makamo wa Rais Solomon Berewa huku kukiwa na hofu kwamba fujo za uchaguzi zinaweza kuikwamisha nchi hiyo yenye kurudi katika hali yake ya kawaida kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Makundi hasimu ya wapiganaji wa zamani yalipambana kwa bunduki na mapamga tokea duru ya kwanza ya uchaguzi hapo Agusti 11 ambapo Koroma wa chama cha APC alishinda kwa asilimia 44 wakati Berewa wa chama cha SLPP alipata asilimia 38 ya kura.

Vituo vya kupigia kura vinatazamiwa kufunguliwa saa moja asubuhi katika nchi hiyo nzima ya Afrika Magharibi yenye idadi ya watu milioni 5.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wametowa wito kwa watu kujitokeza kwa wingi kama ilivyokuwa katika duru ya kwanza ya uchaguzi na kupiga kura kwa amani.