1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Fukuto la mahusiano ya Morocco na Algeria linaongezeka

Sudi Mnette
31 Agosti 2021

Balozi wa Morocco katika Umoja wa Mataifa Omar Hilale, ametoa tamko lenye kuongeza joto dhidi ya Algeria baada ya nchi hiyo kukata rasmi uhusiano wake na Morocco wiki iliyopita,

https://p.dw.com/p/3ziiP
Bildkombo Algerien Präsident Abdelmadjid Tebboune und König Marokko Mohammed VI

Kwa mujibu wa shirika la habari la Morocco, MAP, Omar Hilale, balozi wa Morocco katika Umoja wa Mataifa aliufananisha mzozo wa Morocco juu ya eneo lenye mgogoro la Sahara Magharibi na mzozo wa Algeria juu ya eneo la Kabylie, ambalo watu wa eneo hilo wanapigania haki ya kujitawala.

Kauli yake inaonekana kama yenye kuweza kuichochea Algeria, ambayo juma lililopita litangaza kusitisha mahusiano yake na Morocco pamoja na kwamba hadi wakati huu ofisi za ubalozi za nchi hizo mbili bado zinaendelea kufanya kazi. Kimsingi mpaka kati ya Morocco na Algeria umefungwa tangu mwaka 1994, na Algeria imesema itabadilisha mkondo wa usafirishaji wa bomba la gesi linalopitia katika ardhi ya Morocco.

Utetezi wa eneo linalotaka kujitawala la Kabylie huko Algeria.

Flaggen | Algerien und Marokko | Symbolbild
Picha inayonesha ishaa ya mahusiano yalivyo kati ya Algeria na MoroccoPicha: daniel0Z/Zoonar/picture alliance

Balozi Hilale amenukuliwa akisema watu wa Kabylie pia wana haki ya kujitawala. Na kwa nini Algeria inawanyima haki hiyo na kuidai kwa Wamorocco wa Sahara. Morocco inaitamaza Sahara ya Magahribi  kama sehemu yake, lakini eneo hilo limekuwa katika mzozo wa harakati za Polisario, jitihada ambayo inaungwa mkono na harakati nyingine ya ukombozi ya Algeria, ambayo ilianza tangu wakati wa zama za ukoloni wa Ufaransa katika miaka ya 1970.

Pamoja na kwamba Marekani, imekuwa ikiunga mkono hatua ya Morocco ya juma lililopita la kuirejesha serikali ya Rabat katika kustawisha mahusino ya kidemokrasia na Israel, idadi kubwa za mataifa yamesema yanataka azimio la Umoja wa Mataifa lenye uungwaji mkono wa watu wengine. Zaidi ya mataifa 20, mengi ya hayo yakiwa Kiariabu yamefungua ofisi zao za kibalozi huko Shahara ya Magaribi, ikiwa kuonesha kwa ukamilifu kwaamba wanatambua maamlaka ya Wamorocco.

Algeria imekuwa ikiituhumua Morocco kwa kuliunga mkono kundi lililojulikana kama MAK, ambalo linaendeshwa kutoka Ufaransa, ambalo linaunga mkono uhuru wa eneo la Kabylie la huko kaskazini/mashariki mwa Algeria,linalolaumuiwa kuhusika na janga la moto wa msituni la hivi karibuni.

Miongoni mwa saababu nyingine katika usitishwaji za uhusiano kwa zingatio la msimamo wake kwa eneo la Sahara Magharibi, Algeria imelalamika Morocco kutumia programu ya udukuzi ya Pegasus ya Kiisrael dhidi yake katika kutimiza maelengo yake, jambo ambalo limekanushwa vikali na Morocco kwa kusema sababu hiyo na nyingine zote hazina ukweli.

Chanzo: RTR