1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

G7 wahofia vifaa vya kijeshi vya China kwa Urusi

Saumu Mwasimba
19 Aprili 2024

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa nchi za kundi la G7 wamezungumzia wasiwasi wao kuhusu makampuni ya China kupeleka vifaa vya kijeshi na vipuri vya silaha nchini Urusi kwa ajili ya kulisaidia jeshi la nchi hiyo.

https://p.dw.com/p/4ezHG
Italia | G7
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa wanachama wa kundi la G7 wakiwa mjini Capri, Italia.Picha: Alessandro di Meo/EPA

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken, aliwatolea mwito mawaziri wenzake wa nchi za Umoja wa Ulaya kuongeza shinikizo dhidi ya serikali ya Beijing ambayo Marekani inadai  inaisaidia Urusi kutanuwa jeshi lake tangu enzi za Usovieti.

Soma zaidi: Kundi la G7 lasema Israel ina haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi ya Hamas

Tamko la pamoja la mawaziri hao baada ya kumalizika mkutano wao mjini Capri, Italia, liliitaka China kuhakikisha inasitisha hatua ya kutoa msaada huo kwa Urusi.

Mawaziri hao walisema kuisadia Urusi kujitanua kijeshi ni hatua inayoongeza kitisho kwa majirani wa taifa hilo.