1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gaddafi ataka bunduki aina ya machineguns zipigwe marufuku duniani

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTol

TRIPOLI.Kiongozi wa Libya,Muammar Gaddafi ambaye mwaka 2003 alitaka kuharibiwa kwa silaha za maangamizi ,lakini baadaye akaibuka na kuunga mkono mabomu ya ardhini kwa nchi dhaifu, ameibuka tena safari hii akitaka kupigwa marufuku kwa bunduki za rashasha.

Gaddafi alitoa ombi hilo katika mtandao wake akisema kuwa bunduki hizo za rashasha ambazo kwa kimombo zinajulikana kama machineguns, zimesababisha maafa makubwa kuliko silaha yoyote ile.

Libya ilitia saini mkataba wa kupiga marufuku mabomu ya kutegwa ardhini mnamo mwaka 1997, lakini mwezi uliyopita Gaddafi alisema nchi dhaifu ziruhusiwe kuwa na mabomu hayo kwa ajili ya kujilinda.

Kiongozi huyo wa Libya amezishutumu nchi za magharibi kwa kupandikiza chuki miongoni mwa nchi za kiafrika ili kupata mwanya wa kuiba rasilimali iliyopo.

Ameshadihisha wito wake wa kutaka kuundwa kwa serikali moja ya Afrika itakayokuwa na nguvu ya kuweza kutatua matatizo ya afrika bila ya msaada kutoka nje.