1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gambia yaanza vyema kuelekea michuano ya 2023

Saumu Mwasimba
24 Machi 2022

Timu ya Gambia imeigaragaza Chad kwa bao 1-0 katika hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye michuano hiyo ya mwaka ujao 2023.

https://p.dw.com/p/48ysm
Africa Cup Gambia und Tunesien
Picha: Issouf Sanogo/AFP/Getty Images

Timu ya Gambia iliyotikisa mwaka huu katika soka baada ya kufika kwenye robo fainali ya michuano ya kombe la kuwania ubingwa wa mataifa ya Afrika, siku ya Jumatano imeigaragaza Chad kwa bao 1-0 katika hatua ya kwanza ya kuelekea kwenye michuano hiyo ya mwaka ujao 2023. 

Mchezaji wake Steve Trawally aliifungia Gambia bao dakika ya 89. Kocha wa timu hiyo mzaliwa wa Ubelgiji Tom Saintfiet aliwapa onyo wachezaji wake kabla ya mchuano huo kujiepusha kuwa watu wa kufanya maajabu katika mchezo mmoja tu akiwataka wahakikishe wanafanikiwa kuingia michuano ya kombe la mataifa ya Afrika ya mwaka 2023 na 2025 na pia kombe la dunia 2026.