1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanariadha Gatlin asubiri kupambana Beijing

17 Julai 2015

Mwanariadha Mmarekani wa mbio fupi Justin Gatlin amekiri kuwa adhabu aliyopewa ya kupigwa marufuku ya miaka minne aliyoitumikia kati ya mwaka wa 2006 na 2010 imekuwa “zawadi na pia laana” kwake

https://p.dw.com/p/1G0h8
Justin Gatlin
Picha: picture-alliance/dpa

Gatlin amesema kuimarika kwake katika riadha akiwa na umri wa miaka 33 kunahusikana na hatua ya kufungiwa nje ya mashindnao kwa misimu minne baada ya kupatikana na hatia ya kutumia dawa za kuongeza nguvu mwilini.

Wakati Mjamaica Usain Bolt akiendelea kusumbuliwa na tatizo la nyonga, Mmarekani huyo atashiriki katika mashindano ya ubingwa wa dunia mjini Beijing mwezi ujao akipigiwa upatu kushinda mbio za mita 100 na 200, baada ya kuweka muda bora wa kibinafsi wa 9.74 katika mita 100 mwezi Mei.

Gatlin amesema mwili wake unajihisi kama mtu wa miaka 27 na siyo 33 ambaye amekimbia miaka hiyo minne na kuchoka. Ameongoza kuwa inasikitisha kuwa hakushiriki mashindano, lakini aliweza kupumzika na kuwaona wapinzani wake wakiimarika.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/AP/DPA
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman