1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gauck ateuliwa kugombea urais wa Ujerumani

20 Februari 2012

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amekubali kumuunga mkono mwanaharakati wa kutetea haki za kiraia kutoka iliyokuwa Ujerumani Mashariki, Joachim Gauck, kuwa rais mpya.

https://p.dw.com/p/145rS
Berlin/ Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) stellt am Sonntag (19.02.12) in Berlin nach einem Gespraech im Kanzleramt in Berlin auf einer Pressekonferenz den Theologen und ehemaligen Leiter der Stasi-Unterlagenbehoerde, Joachim Gauck, als Kandidaten fuer das Bundespraesidentenamt vor. Die Spitzen der Regierungsparteien und Vertreter von SPD und Gruenen einigten sich am Sonntag auf Gauck als Kandidaten fuer das Bundespraesidentenamt. (zu dapd-Text) Foto: Steffi Loos/dapd
Pressekonferenz im Bundeskanzleramt BundespraesidentPicha: dapd

Kuteuliwa kwa Joachim Gauck hapo jana kulikuja baada ya kansela Merkel na muungano wake wa vyama vya Christian Democratic Union, CDU na Christian Social Union, CSU, kufutilia mbali upinzani wao dhidi ya mgombea huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 72. Hatua ya Merkel imeumaliza mzozo wa kisiasa ambao ulikuwa umeanza kumtia katika kiti moto.

Merkel ambaye kama Gauck alikulia Ujerumani Mashariki na ni Mprotestanti, alimpongeza mchungaji huyo kama mwalimu halisi wa demokrasia aliyesaidia nchi kuungana pamoja tangu muungano mwaka 1990. "Mada muhimu katika kazi ya Joachim Gauck ni wazo la uhuru katika kutekeleza majukumu. Hilo ndilo binafsi linaloniunganisha naye, mbali na tofauti nyengine zilizopo kati yetu."

Bi Merkel aidha alisema Gauck anaweza kuleta ari mpya katika kukabiliana na changamoto zinazoikabili Ujerumani kwa wakati huu na kutoa mchango muhimu kwa mustakabali wa taifa.

Berlin/ Der Theologe und ehemalige Leiter der Stasi-Unterlagenbehoerde, Joachim Gauck, sitzt am Sonntag (19.02.12) im Kanzleramt in Berlinauf einer Pressekonferenz der Spitzen der Regierungsparteien und Vertretern von SPD und Gruenen zur Vorstellung des Kandidaten fuer das Bundespraesidentenamt auf dem Podium. Die Spitzen der Regierungsparteien und Vertreter von SPD und Gruenen einigten sich am Sonntag auf Gauck als Kandidaten fuer das Bundespraesidentenamt. (zu dapd-Text) Foto: Steffi Loos/dapd
Joachim GauckPicha: dapd

Gauck alikuwa mgombea wa vyama vya upinzani vya Social Democratic, SPD, na Kijani mwezi Juni mwaka 2010 dhidi ya Christian Wulff, waziri mkuu wa zamani wa jimbo la Lower Saxony alikuwa chaguo la Merkel kwa wadhifa wa urais ambao ni wa heshima.

Upinzani ulimpendekeza tena Gauck kufuatia uamuzi wa Wulff kujiuzulu. Chama pekee cha mrengo wa shoto cha Die Linke, kinachowajumuisha mafashsti wa iliyokuwa Ujerumani Mashariki, kimesema hakitamuunga mkono bwana Gauck atakapopigiwa kura mwezi ujao. Ushindi wa Gauck ni wa hakika huku kukiwa na idadi kubwa ya wajumbe katika baraza la wawakilishi litakalomchagua rais, kwa maana kwamba Wajerumani wawili kutoka Ujerumani Mashariki watakalia nyadhifa muhimu zaidi za kisiasa nchini.

Akizungumza baada ya uteuzi wake, Gauck alisema ametunukiwa heshima kubwa. "Hii ni siku maalumu sana kwangu, hata katika maisha ambayo nimekuwa na siku kadhaa muhimu. Kinachonisisimua zaidi ni mtu kama mimi aliyezaliwa wakati wa vita vibaya na aliyeishi miaka 40 chini ya utawala wa kidikteta, anapaswa kuombwa leo hii awe kiongozi wa dola."

Hata hivyo Gauck, ambaye si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa, alikiri amefurahi na kuchanganyikiwa kidogo kwa kuwa mchezo wa kisiasa wa soka katika kipindi cha miaka miwili.

Mwenyekiti wa chama cha SPD, Sigmar Gabriel, amesema baada ya uteuzi wa Gauck kwamba "kila kitu kinachomalizika vizuri ni salama".

Mwandishi: Josephat Charo/AFPE

Mhariri: Mohammed Abdulrahman