1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA CITY : Mapigano yaendelea licha ya suluhu

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1B

Takriban watu 20 wameuwawa wakati mapambano kati ya makundi hasimu ya Kipalestina ya Hamas na Fatah yakiendelea katika Ukanda wa Gaza.

Mapigano hayo yanakuja licha ya kuwepo kwa makubaliano mengine ya kusitisha mapigano ambayo ni makubalino ya nne kati ya makundi hayo.Idadi ya vifo kutokana na mapigano hayo ya karibuni yaliozuka mwishoni mwa juma imepindukia watu 40.

Mapigano hayo kati ya Hamas na Fatah ni mabaya kabisa kuwahi kushuhudiwa tokea makundi hayo mawili yaunde serikali ya umoja wa kitaifa miezi miwili iliopita.

Wakati huo huo Israel imefanya mashambulizi mawili ya anga na kuuwa watu wanne.Mojawapo ya eneo lililoshambuliwa ni kambi ya mafunzo ya Hamas kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.

Israel hapo jana imesema itachukuwa hatua kali dhidi ya wanamgambo wa Kipalestina huko Gaza ambao wamevurumisha maroketi kadhaa katika miji ya Israel ilioko karibu katika siku za hivi karibuni.