1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Machafuko ya Gaza yasababisha wasiwasi

17 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC1I

Jumuiya ya kimataifa ina hofu kuwa mapigano makali yanayoendelea kati ya Hamas na Fatah, huenda yakahatarisha serikali ya umoja iliyoundwa hivi karibuni na makundi hayo mawili ya Kipalestina.Umoja wa Ulaya na Marekani zimetoa mwito wa kukomesha mapigano kati ya Hamas na Fatah.Ujerumani ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa urais wa Umoja wa Ulaya,imeziomba Saudi Arabia na Misri zijaribu kuyapatanisha makundi mawili ya Wapalestina yanayohasimiana.Zaidi ya watu 40 wameuawa tangu mapambano mapya kuzuka mwishoni mwa juma lililopita.Kwa upande mwingine si chini ya watu 4 wameuawa katika mashambulio mawili ya angani yaliyofanywa na Israel.Shambulizi moja lililenga jengo lililokuwa likitumiwa na Hamas mjini Rafah.Mashambulio hayo yamefanywa baada ya wanamgambo wa Kipalestina kurusha makombora katika mji wa Sderot,kusini mwa Israel.