1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina 7 wauawa katika Ukanda wa Gaza

13 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CBJX

Mapambano mapya kati ya vyama vya Kipalestina vya Hamas na Fatah,yamesababisha umwagaji mpya wa damu katika Ukanda wa Gaza.Hadi watu 7 wameuawa na wengine 85 wamejeruhiwa baada ya polisi wa Hamas na wanamgambo waliojificha nyuso kuwafyatulia risasi waandamanaji waliokusanyika kumkumbuka kiongozi wa zamani wa Wapalestina, Yasser Arafat aliefariki miaka mitatu iliyopita. Kiasi ya wafuasi 250,000 wa Fatah walimiminika kwenye Ukanda wa Gaza unaodhibitiwa na Hamas. Tangu mwezi wa Juni,eneo hilo linadhibitiwa na Hamas baada ya kukitimua chama cha Fatah cha Rais Mahmoud Abbas.