1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA: Wapalestina wazindua mpango mpya wa usalama.

10 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3U

Mamia ya polisi wa Palestina wamezindua mpango mpya wa usalama ili kurejesha utangamano katika eneo hilo.

Hiyo ndiyo mara ya kwanza ambapo makundi hasimu ya Fatah na Hamas yameungana kushughulikia usalama.

Msemaji wa Rais Mahmoud Abbas wa chama cha Fatah amesema maafisa wa usalama watavaa sare na watapokea maagizo kutoka wizara ya mambo ya ndani.

Mpango huo wa kiusalama umelengwa kukabiliana na mzozo kati ya makundi hayo mawili.

Mwaka uliopita watu karibu ya mia nne waliuawa kwenye ghasia kati ya wafuasi wa vyama hivyo viwili.