1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GAZA:Ripota Johston wa BBC hatarini?

18 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBqm

Kundi la kipalestina linalojiita jeshi la Uislam limetishia kumwuua ripota wa shirika la Utangazaji la Uingereza BBC Alan Joshston. Vitisho hivyo vimetangazwa katika ukanda wa video ulioneshwa na shirika la televisheni, Al-Jazeera.

Bwana Johston alitekwa nyara kwenye Ukanda wa Gaza miezi mitatu iliyopita. Hapo awali kulikuwa na habari juu ya mwandishi huyo kuachiwa baada ya mapatano kufikiwa. Lakini wanaomshikilia wamesema hakuna mapatano yoyote.