1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia zaidi zaendelea Ufaransa

27 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CTiU

PARIS.Polisi nchini Ufaransa kwa siku ya pili mfululizo wameendelea kupambana na waandamanaji katika ghasia zilizolikumba eneo la kaskazini mwa Paris.

Polisi walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi pamoja na risasi za mpira kutuliza ghasia.

Vijana wenye hasira waliendelea kufanya ghasia kwa kuwashambulia polisi, huku wakiharibu magari na majengo kwenye kitongoji cha Villiers-le-Bel.

Zaidi ya polisi 64 walijeruhiwa katika ghasia hizo, watano wakiwa katika hali mbaya.Chanzo cha ghasia hizo ni vifo vya vijana wawili waliyogongwa na gari ya polisi Jumapili iliyopita.