1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ghasia zimeendelea Ufaransa usiku wa tatu kwa mfululizo

28 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CU8k

Machafuko yaliendelea kwa usiku wa tatu kwa mfululizo katika vitongoji vya mji mkuu wa Ufaransa,Paris.Machafuko hayo sasa yamefika mji wa kusini wa Toulouse ambako polisi wamesema magari 10 yamertiwa moto pamoja na maktaba moja. Hata hivyo,machafuko hayo hayakufikia kiwango cha ghasia za siku mbili zilizopita ambapo zaidi ya polisi 80 walijeruhiwa.Sasa polisi wameimarishwa katika maeneo hayo ya machafuko.Rais Nicolas Sarkozy ametoa mwito wa kuwa na utulivu.Hii leo ana mkutano wa dharura pamoja na waziri mkuu na baraza la mawaziri.