1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Glascow. Uwanja wa ndege wafungwa.

1 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBmr

Uwanja wa ndege wa mjini Glasgow nchini Scotland umefungwa baada ya gari moja kugonga eneo kuu la kuwasili kwa wasafiri na kulipuka moto. Mkuu wa polisi wa mji wa Glasgow Willie Rae amesema tukio hilo linachukuliwa kuwa ni shambulio la kigaidi, linalohusiana na jaribio la siku ya Ijumaa la shambulio la bomu mjini London.

Amesema kuwa hakukuwa na taarifa za kijasusi kabla ya tukio hilo, ambazo zilionyesha kuwa Scotland itashambuliwa. Hata hivyo ameongeza kuwa kutokana na tukio la mjini London kumekuwa na mazungumzo ya karibu na kitengo cha ujasusi cha M 15 pamoja na juhudi za polisi na majeshi yote nchini.

Polisi wamewakamata watu wawili baada ya tukio hilo.

Mmoja kati ya watu hao wawili amelazwa hospitali akiwa na majeraha makubwa ya kuungua.

Anasemekana kuwa yuko katika hali mbaya.

Kuna taarifa zisizothibitishwa kuwa mtuhumiwa wa tatu aliuwawa katika shambulio hilo.

Mtu mmoja aliyekuwa karibu anapatiwa matibabu kutokana na majeraha aliyoyapata.

Polisi wanasema hakuna mtu mwingine aliyeathirika.

Safari zote zimefutwa hadi itakapotangazwa tena.

Uwanja wa ndege wa Liverpool pia umefungwa hadi itakapotangazwa tena huku kukiwa na hofu ya kutokea mashambulizi mengine.