1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GLASGOW: Mshukiwa wa shambulizi amefariki hospitali

3 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBcj

Mtuhumiwa mmojawapo kuhusika na jeribio la shambulizi la bomu kwenye uwanja wa ndege wa Glasgow amefariki hospitalini.Kafeel Ahmed aliekuwa akilindwa hospitali na polisi wenye silaha,alipata majeraha mabaya ya moto,katika shambulizi hilo kwenye uwanja mkubwa kabisa wa Scotland hapo tarehe 30 mwezi Juni.Ahmed alikuwa dreva wa gari lililopakiwa miripuko na kubamizwa kwenye kituo cha abiria wa ndege na kushika moto.