1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GOMA:Hali ya usalama yazidi kuzota mashariki ya Kongo

7 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Hu

Hali ya usalama inazidi kuzorota mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo.Wanajeshi wa serikali waliwauwawa waasi 38 wafuasi wa generali muasi Laurent Nkunda wakati wa mapigano makalai hapo jana mashariki mwa eneo la Kivu Kaskazini.

Kwa mujibu wa afisa wa jeshi la serikali Meja Joseph Kabuyaya waasi 38 waliuwawa na wengine wengi walijeruhiwa na kupelekwa katika kambi ya jeshi.Mapigano yalianza jumamosi asubuhi katika mbuga ya wanyama ya Virunga ambako ni maficho ya wapiganaji wa Nkunda.