1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Gordon Brown atagangaza baraza lake la mawaziri

Abdu Mtullya28 Juni 2007

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza Gordon Brown ametangaza baraza lake la mawaziri akiwamo bibi Jacqui Smith ambaye ni mwanamke wa kwanza katika wadhifa wa waziri wa mambo ya ndani.

https://p.dw.com/p/CB3E
Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Uingereza, David Miliband
Waziri mpya wa mambo ya kigeni wa Uingereza, David MilibandPicha: AP

Waziri mkuu Brown amefanya kikao cha kwanza na baraza lake la mawaziri leo alasiri muda mfupi baada ya kulitangaza baraza hilo lenye sura mpya nyingi ikiwa pamoja na ya David Miliband atakaekuwa waziri wa mambo ya nje.

Waziri Miliband mwenye umri wa miaka 41 anaweka rekodi ya kuwa waziri wa mambo ya nje kijana kuliko wote tokea wakati wa David Owen mnamo mwaka 1977.

Wizara ya maendeleo ya kimataifa itakuwa chini ya Douglas Alexander.

Aliewahi kuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya Tony Blair bwana Jack Straw amerudishwa tena katika baraza la mawaziri la serikali ya leba. Sasa atakuwa waziri wa sheria.

Badiliko kubwa katika baraza hilo ni uteuzi wa bibi Jacqui Smith, mwanamke wa kwanza atakaekuwa waziri wa mambo ya ndani.

Na waziri mpya wa fedha sasa atakuwa Alistair Darling.

Waziri Mkuu Brown ameahidi kufanya mabadiliko ili kuweza kutekeleza sera anazozipa kipaumbele. Sura nyingi mpya katika baraza lake la mawaziri zinathitibisha dhamira yake katika ,kuleta mabadiliko kama alivyositiza mwenyewe kabla ya kuingia ofisini namba 10 downing street.

AM.