1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

GUANTANAMO: Mahabusu ajinyonga

31 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwM

Majeshi ya Marekani yamesema mahabusu wa Saudi Arabia amejinyonga katika gereza la Guantanamo Bay, Cuba.

Uchunguzi umeanzishwa kuhusu tukio hilo.

Mahabusu huyo amejiua siku mbili kabla ya wafungwa wengine wawili kuwasilishwa mbele ya mahakama ya kijeshi ya uhalifu wa kivita.

Mwaka uliopita raia wawili wa Saudi Arabia na mmoja wa Yemen walijinyonga katika gereza hilo.

Gereza hilo lina wafungwa kiasi mia tatu na themanini ambao wamekuwa wakishikiliwa kwa miaka mitano bila haki ya kupinga kuzuiliwa kwao.

Marekani inasema wafungwa hao hawalindwi na mkataba wa Geneva unaowashughulikia wafungwa wa kivita.