1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Guatemala City. Bush akumbana na maandamano zaidi katika ziara yake.

12 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJw

Rais wa Marekani George W. Bush amewasili nchini Guatemala baada ya ziara ya saa sita katika mji mkuu wa Colombia , Bogota akiwa katika ziara ya mataifa matano ya Latin Amerika. Mkutano wake na rais wa Colombia Alvaro Uribe, mshirika wake wa karibu katika bara hilo la Amerika ya kusini , ilikumbana na maandamano makubwa licha ya hatua kali za ulinzi.

Katika hotuba yake kwa rais wa Colombia, Bush alimtaja rais huyo kuwa ni rafiki yake wa karibu.

Waandamanaji walichoma bendera za Marekani, walivunja madirisha ya maduka na bishara mbali mbali na kupambana na polisi.

Maelfu ya polisi na wanajeshi waliwekwa kwa ajili ya ziara hiyo fupi, baada ya ziara za Bush huko Brazil na Uruguay ambako pia kumekuwa na maandamano makubwa.

Maandamano mengine yanatarajiwa , wakati rais Bush akielekea huko Guatemala na Mexico. Bush hakujali matamshi makali kutoka kwa rais wa Venezuela Hugo Chavez, ambaye nae yuko katika ziara katika eneo hilo.