1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Götze kujiunga na Eintracht Frankfurt

20 Juni 2022

Mabingwa wa Ligi ya Ulaya Europa League Eintracht Frankfurt wanakaribia kumsajili kiungo wa zamani wa Borussia Dortmund na Bayern Munich Mario Götze kutoka PSV Eindhoven ya Uholanzi.

https://p.dw.com/p/4CxXN
Fussball I Mario Goetze I PSV Eindhoven
Picha: NESImages/vi/DeFodi Images/picture alliance

Inadaiwa kwamba Götze ameshakubaliana masuala ya kimshahara na Frankfurt na kocha wa klabu hiyo Oliver Glasner tayari ameshafanya mazungumzo na Götze mwenyewe.

Inaripotiwa kwamba mazungumzo ya usajili huo yako katika hatua za mwisho na Frankfurt watalipa yuro milioni 4 kwa ajili ya huduma zake.

Götze mwenye umri wa miaka 29 aling'aa sana katika kipindi cha kwanza alipokuwa Borussia Dortmund ila alipohamia Bayern Munich akapitia wakati mgumu na aliporudi tena Dortmund mambo hayakumwendea vizuri na akaishia kuhamia PSV.