1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali mbaya ya maisha katika Gaza yashtusha

16 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D8Zk

GAZA:

Mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja wa Mataifa,John Holmes amesema , ameshtushwa mno na hali mbaya ya maisha aliyokuta katika Ukanda wa Gaza. Amesema,vikwazo vilivyowekwa na Israel baada ya kundi la Hamas kudhibiti eneo hilo miezi minane iliyopita,vimesababisha hali mbaya ya maisha.

Holmes,amepelekwa Gaza kutoa mapendekezo kwa Israel na Mamlaka ya Wapalestina kuchukua hatua ili kupunguza dhiki za wakazi katika Ukanda wa Gaza.

Kama Wapalestina milioni 1.4 wanaishi katika Ukanda wa Gaza.Israel inasema, imechukua hatua hiyo kujibu mashambulizi ya makombora yanayofanywa kutoka eneo la Gaza yakilenga miji ya kusini mwa Israel.