1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali tete yajitokeza Komoro kufuatia kuuwawa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais

Josephat Nyiro Charo14 Juni 2010

Kanali Kombo Ayuba alipigwa risasi na kuuwawa wakati akishuka kutoka kwenye gari lake nyumbani kwake

https://p.dw.com/p/NqXb

Mkuu wa kikosi cha ulinzi wa Rais Ahmed Abdullah Sambi katika visiwa vya Comoro Kanali Kombo Ayuba amepigwa risasi na kuuwawa. Kanali huyo alipigwa mlolongo wa risasi wakati akishuka garini nyumbani kwake katika mji mkuu Moroni.

Aboubakar Liongo alizungumza kwa njia ya simu na mchambuzi na mhadhiri katika chuo kikuu cha Comoro, Profesa Ibrahim Mohamed Ibrahim ambaye kwanza alinieleza juu ya hali ilivyo wakati huu baada ya tukio hilo.

Mahojiano:Liongo/Prof Ibrahim Mohamed

Mpitiaji:Abdul-Rahman