1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali wilayani Bududa, Uganda baada ya maporomoko ya ardhi

4 Machi 2010

<p>Juhudi za kutafuta miili ya watu waliofariki kutokana na maporomoko ya ardhi wilayani Bududa nchini Uganda bado zinaendelea, licha ya kukumbwa na changamoto kadhaa, ikiwemo uduni wa vifaa wanavyotumia.</p>

https://p.dw.com/p/MJRc
Waokoaji wapo kazini kutafuta miili ya watuPicha: picture-alliance/Photoshot

Hali hiyo pia inatokana na ukosefu wa barabara za kupitisha mashine nzito kama vile greda.

Mwandishi wetu nchini Uganda, Leylah Ndinda, ambaye ametembelea eneo hilo, anaarifu kuwa shughuli za uchimbaji zilisitishwa jana jioni na mvua kubwa iliyonyesha, hali iliyosababisha watu kulimbia eneo la tukio wakihofia

 kutokea tena kwa maporomoko ya ardhi.

Leylah Ndinda anaeleza zaidi hali ilivoyo kwa sasa katika eneo hilo.

Mwandishi: Leyla Ndinda Mhariri: Othman Miraji