1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hali ya afya ya rais Buhari nzuri

Sekione Kitojo
16 Februari 2017

Kiongozi wa baraza la Seneti nchini Nigeria amesema kwamba Rais Muhammadu Buhari yuko katika hali nzuri kiafya mjini London, akijaribu kutupilia mbali uvumi juu ya hali ya afya ya rais huyo

https://p.dw.com/p/2XgOp
Paris Medef Zentrale Buhari Gattaz
Picha: Getty Images/AFP/E. Piermont

Bukola Saraki jana  alikwenda  katika mji mkuu  wa Uingereza pamoja na kiongozi wa  wajumbe walio wengi katika baraza la Seneti, Ahmed Lawan, na spika  wa baraza la wawakilishi, Yakub Dogora. Ni ujumbe wa hivi karibuni kabisa wa  kisiasa  kumtembelea kiongozi huyo mwenye  mri wa miaka 74 katika makaazi rasmi ya ubalozi wa Nigeria nchini  Uingereza, ambako amekuwa akiishi kwa karibu mwezi mmoja. Saraki amesema katika taarifa kwenye ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Facebook  kwamba Buhari yuko katika hali nzuri kiafya, na hakuna sababu ya  wasiwasi. Katika ukurasa wa Twitter Buhari ameandika   jana kwamba amefurahishwa na ziara hiyo na  kuwashukuru Wanigeria, Wakristo na Waislamu kwa dua zao na kumtakia kheri ya afya njema.