1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG: Hukumu ya mshukiwa wa mashambulio ya Septemba 11 kutolewa leo

8 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCcP

Raia wa Moroko aliyeshtakiwa kuhusiana na mashambulio ya Septemba 11 nchini Marekani anatarajiwa kuhukumiwa leo na majaji wa hapa Ujerumani.

Mounir el Motassadeq, mwanamume wa kwanza kushtakiwa kuhusiana na mashambulio hayo, anatarajiwa kuhukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani wakati kesi yake itakaposikilizwa kwa mara ya tatu.

Kwa sasa Motassadeq anatumikia kifungo cha miaka saba jela. Alishtakiwa kwa kuwa mwanachama wa kundi la kigaidi na kutumiwa kama chombo cha mauaji ya abiria waliokuwa kwenye ndege za abiria zilizotekwa nyara.

Ijumaa iliyopita, Motassadeq alikanusha mashtaka dhidi yake akisisitiza hakujua lolote kuhusu njama ya mashambulio dhidi ya Marekani.