1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HAMBURG: Utulivu umerejea baada ya ghasia za wanaharakati

29 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBwz

Hali ya utulivu imerejea katika barabara za mji wa Hamburg nchini Ujerumani, baada ya wapinzani wa utandawazi kupambana na polisi siku ya Jumatatu. Ghasia zilizuka baada ya polisi kurushiwa chupa na mawe na wandamanaji walioweka vizuizi barabarani.Polisi walitumia maji na virungu kupambana na machafuko hayo na watu 24 walikamatwa.Wapinzani wa utandawazi walifanya maandamano yao siku ya kwanza ya mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa masuala ya nje wa Umoja wa Ulaya na nchi za Asia.Wandamanaji hao wanapinga mkutano wa kilele wa nchi tajiri duniani zilizoendelea kiviwanda G-8 utakaofanywa mjini Heiligendamm nchini Ujerumani kuanzia tarehe 6 hadi 8 Juni.Mkutano huo wa kilele utaongozwa na Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ambayo hivi sasa imeshika wadhifa wa urais katika Umoja wa Ulaya.