1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

HANOI.Viongozi walekea Hanoi kwa mkutano wa kilele wa maswala ya biashara

15 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCse

Wajumbe kutoka mataifa 21 wanakusanyika katika mji wa Hanoi nchini Vietnam tayari kujiandaa kwa mkutano wa kilele wa viongozi utakaojadili maswala ya uchumi wa maeneo ya Asia na Pacifik – APEC- mwishoni mwa wiki hii.

Mkutano huo utajishughulisha zaidi na mzozo wa biashara ulimwenguni na tamaa ya Korea Kaskazini ya kudhibiti nyuklia.

Rais George W Bush wa Marekani ambae yuko njiani kuelekea Hanoi amesema.

O ton…Jambo moja kati ya mambo nitakayo zungumza na washirki wa mkutano wa APEC ni kuhusu biashara huru lakini ya haki. Na ujumbe wangu kwa washiriki wenzetu katika biashara ni kwamba tutendeeni yale tunayowatendea, masoko yetu yako wazi kwa bidhaa zenu nanyi masoko yenu yawe wazi kwetu.

Rais Bush amewasili mjini Moskow, Urusi ambako atasimama kwa muda mfupi na pia atapitia Singapore na Indonesia kabla ya kuwasili mjini Hanoi.

Marais Vladmir Puttin wa Urusi, na Hu Jiantao wa China wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo akiwemo waziri mkuu mpya wa Japan Shinzo Abe.

Mkuu wa shirika la biashara duniani Pascal Lamy tayari ameshawasili mjini Hanoi.