1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatima ya Mazungumzo ya Amani Mashariki ya Kati baada ya Aprili 29

29 Aprili 2014

Muda uliowekwa na Marekani wa kufanya mazungumzo ya kuleta suluhisho la mgogoro wa Mashariki ya Kati umemalizika na hakuna dalili ya kusonga mbele. Hata hivyo John Kerry amesema mchakato wa amani bado uhai.

https://p.dw.com/p/1BqcG
Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiamkiana na kiongozi wa utawala wa ndanai wa Palastina Mahmoud Abbas,septemba mwaka 2010Picha: picture-alliance/dpa

Baada ya kushindikana kwa juhudi thabiti za kidiplomasia zilizochukua muda wa zaidi ya mwaka mmoja kwa lengo la kuleta suluhisho la mgogoro wa mashariki ya kati hadi kufikia leo ,subira ya mpatanishi-Marekani imezidi kupungua kutokana na Israel na Wapalestina kujiweka kando ya juhudi za mazungumzo.

Lakini Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry bado ameeleza matumaini kwa kusisitiza kwamba mchakato wa mazungumzo ya kuleta amani katika mashariki ya kati bado haujazimika. Hata hivyo Waziri Kerry ameeleza kuwa mchakato huo umeingia katika hatua ya makabiliano , katika upande mmoja na mkwamo katika mwingine.

Lakini pande zote kuu za mchakato wa masharriki ya kati, Israel na Wapalestina zimeshafanya maamuuzi yao .

Kufuatia makubaliano yaliyofikiwa baina ya pande mbili za Wapalestina,Hamas na Fatah ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa,Israel imeamua kuyavunja mazungumzo.

Israel haina njia nyengine,lakini suluhisho la muda linahitajika

Mtafiti kwenye taasisi ya masuala ya usalama ya mjini Telaviv Mark Heller amesema uamuzi wa Israel wa kuyavunja mazungumzo na Wapalestina unaweza kueleweka.Mark Hall ameeleza kwamba haina maana kwa Israel kufanya mazungumzo ikiwa upande mmoja hautaki.Hata hivyo mtaalamu huyo ameshauri kwamba madhali mazungumzo yamesimama, inapasa kutafuta suluhisho la muda.Ameeleza.Watu wengi wana maoni kwamba, pamoja na kufanya juhudi za kuuendeleza mchakato wa mazungumzo ya kuleta amani, hatua nyingine zinaweza kuchukuliwa, kama suluhisho la mpito.

John Kerry Tel Aviv 01.04.2014
Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry ziarani mjini Tel Aviv mapema m,wezi wa AprilPicha: Reuters

Kwa mfano ingefaa kuyahamishia kwa mamlaka ya Wapalestina madaraka ya utawala ya sehemu za Wapalestina zinazodhibtiwa sasa na Israel."

Waziri Mkuu w a Israel Benjamin Netanyahu amesema hakuna mazungumzo yatakayofanyika baina ya Israel na serikali yoyote mpya ya Wapalestina mpaka hapo Hamas itakapoitambua Israel.

John Kerry akanusha tuhuma za kuilinganisha Israel na nchi ya kibaguzi

Wakati huo huo Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John kerry amekanusha vikali, kuifananisha Israel na iliyokuwa serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini. Baada ya kutolewa miito mikali ya kumtaka ajiuzulu, au angalau aombe radhi, Kerry amesema haamini iwapo alisema hadharani au kwa faragha kuwa serikali ya Isreal ni ya kibaguzi kama ile ya Afrika Kusini ya hapo awali.

Benjamin Netanyahu im Kabinett in Jerusalem
Waziri mkuu wa Israel na baraza lake la mawaziriPicha: picture-alliance/dpa

Lakini mjumbe mkuu wa Wapalestina kwenye mazungumzo na Israel Saeb Erakati ameilaumu Israel. Erakat amesema ikiwa amani haiwezi kufikiwa bila ya ushiriki wa Gaza, na kwa hakika haiwezi kufikiwa bila ya Ukanda wa Gaza, basi Israel inalenga shabaha nyingine, yaani ya kutofikia amani.

Lakini mbunge mmoja wa Israel, Tzahi HaNegbi aliepo karibu na Waziri Mkuu Netanyahu ameimbia radio ya jeshi kwamba Israel inapasa kusubiri na kuielewa maana ya makubaliano yaliyofikiwa baina pande mbili za Wapalestina.

Mwandishi:Mtullya abdu/afpe

Mhariri.Hamidou Oummilkheir