Hatimaye Jenerali muasi Laurent Nkunda akamatwa
23 Januari 2009Matangazo
Kiongozi huyo wa kundi la waasi wa CNDP Laurent Nkunda amekamatwa nchini Rwanda alipokuwa akijaribu kutoroka wakati wa operesheni ya pamoja ya kijeshi kati ya majeshi ya Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo dhidi ya wapiganaji wa kihutu wa FDLR.
Nkunda alikamatwa jana usiku kwenye mpaka wa Rwanda na Kongo wakati majeshi hayo yalipovamia ngome ya kundi la CNDP.
Maelezo zaidi anatuletea mwandishi wetu wa Goma John Kanyunyu