Hatimaye matumaini ya kuokolewa.
9 Oktoba 2010Matangazo
SAN JOSE:
Wachimba migodi 33 walionaswa chini ya mgodi sasa wamefikiwa na mtaimbo.
Mtaimbo huo ulichimba na kuingia katika sehemu waliponaswa wafanyakazi hao umbali wa futi alfu mbili chini ya ardhi. Na sasa itawezekana kutengeneza upenyo utakaowezesha kuteremsha kitasa maalumu kitakachowapakia watu hao na kuwafikisha juu ya ardhi. Mlio wa king'ora ulioashiria kufaulu kwa juhudi za kuwafikia wachimba migodi hao uliwapa faraja watu hao pamoja na ndugu zao nchini Chile kote.
Rais Sebastian Pinera wa Chile amesema, kile ambacho kingeliweza kuwa msiba sasa kimegeuka kuwa neema.Watu hao sasa wanatarajiwa kuuona tena mwanga wa jua katika muda wa siku chache zijazo.