1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Hatua za usalama za imarishwa nchini Uengereza

Oummilkheir30 Juni 2007

Bomu la pili lateguliwa mjini London ambako viongozi wanahofia Al ´Qaida wako nyuma ya njama hizo zilizoshindwa

https://p.dw.com/p/CB39
Picha: AP

London:

Juhudi za kuwasaka waasisi wa njama iliyoshindwa ya mashambulio ya mabomu mjini London zimeshika kasi nchini Uengereza.Polisi imesambaza picha kadhaa za watuhumiwa zilizonaswa na kamera katika eneo mashuhuri la Piccadilly Circus mjini London.Wawakilishi wa idara za usalama na mawaziri wa serikali ya waziri mkuu mpya Gordon Brown wamepangiwa kukutana hii leo kuzungumzia hatua zaidi zinazobidi kuchukuliwa.Jana polisi waliyategua mabomu mawili yaliyofichwa ndani ya magari mjini London-mabomu ambayo yangeripuka yangeweza kugharimu maisha ya mamia ya watu.Maafisa wa usalama wanaamini magaidi wa al Qaida wako nyuma ya njama hizo.

Mkuu wa idara ya kupambana na visa vya kigaidi katika Scotland Yard,Peter Clarke anasema:

„Tunafanya kila liwezkanalo kuihifadhi jamii.Polisi zaidi watapiga doria.Utafiti unasonga mbele.Kugunduliwa bomu la pili ni kishindo chengine kinachotufanya tuzidi kua macho.“

Hofu zimezidi nchini Uengereza ambako wananchi wanaadhimisha miaka miwili tangu mashambulio ya mabomu ya mjini London yaliyogharimu maisha ya watu 52.