1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Heiligendam, Ujerumani. Viongozi waafikiana kuhusu upunguzaji wa gesi za sumu.

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBtu

Katika mkutano wa kundi la mataifa yenye utajiri mkubwa wa viwanda G8 mjini Heiligendamm nchini Ujerumani , viongozi wa mataifa hayo wamekuwa wakihangaika kutafuta njia ya kupata makubaliano juu ya kupambana na ongezeko la hali ya ujoto duniani.

Waziri mkuu wa Uingereza Tony Blair amesema kuwa makubaliano hayatakuwa na viwango maalum kwa ajili ya pukunguza gesi zinazoharibu mazingira. Maelezo ya Blair yanaakisi maelezo ya hapo kabla ya rais wa Marekani.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel , ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo wa G8 amekuwa akisisitiza kupatikana malengo maalum ya kupunguza utoaji wa gesi hizo zinazochafua mazingira, na amesema amefurahishwa na kwamba viongozi sasa wanatambua athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Wakati huo huo , rais wa Marekani George W. Bush anataka kupunguza hali ya wasi wasi na rais wa Russia Vladimir Putin. Katika maelezo yake kabla ya mkutano wa viongozi hao , Bush amesema kuwa mzozo na Russia juu ya pendekezo la kuweka mfumo wa ngao dhidi ya makombora katika bara la Ulaya hauna maana kwa upande wowote kuuendeleza.